BOUSSIA DORTMUND YANENA JAMBO KUHUSU KUMUUZA PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG


Boussia Dortmund inaumana na Tottehanm Jumanne hii katika mechi ya Champions League ambapo moja ya mambo yatakayowapa nguvu miamba hiyo ya Ujerumani, ni kurejeshwa kwa mshambuliaji  Pierre-Emerick Aubameyang.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Gabon, aliondolewa kikosini pale Dortmund ilipomenyana na Stuttgart kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Ujerumani, Ijumaa usiku, sababu kuu ikiwa ni utovu wa nidhamu.

Mtendaji wa Dortmund, Hans-Joachim Watzke amethibitisha kuwa nyota huyo ataikabili Tottenham.

Hans-Joachim Watzke amesema tetesi usajili zilizoibuka baada ya klabu hiyo kumwadhibu Aubameyang, ni za kupuuzwa tu.

Amedai hawana mpango wa kumuuza nyota huyo dirisha la Januari na kwamba kilichotokea, ni sehemu tu ya kuimarisha nidhamu klabuni.

No comments