CANNAVARO: PRISONS JIANDAENI, SASA ZAMU YENU KUNYOLEWA

NAHODHA wa timu ya Yanga, Nadir Haroub “Cannavaro” amesema kuwa kikosi cha timu ya Tanzania Prisons nacho kijiandae kukumbana na kipigo kikubwa katika mchezo unaofuata wa Ligi Kuu bara.

Yanga watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya Jumamosi wakati Simba wataikaribisha Lipuli ya Iringa Jumapili katika mfululizo wa Ligi Kuu jijini Dar es Salaam.

Mechi hizi zinatarajiwa kucheza kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi ili kupisha shughuli za kijamii katika uwanja wa Uhuru.

“Hata msimu uliopita tulianza taratibu lakini baadae tulichanganya na kubeba ubingwa kwa staili ya kushangaza watu, hivyo kwa sasa tuko kwenye kiwango tulichokuwa tunakitaka,” alisema beki huyo.

“Tunahitaji kuendeleza ushindi kwa idadi kubwa ya mabao ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa, nadhani timu inayofuata itarajie kukutana na kitu cha kushangaza,” aliongeza.


Yanga iliifunga timu ya Mbeya City kwa mabao 5-0 na hivi sasa inatarajia kucheza na ndugu zao, Tanzania Prisons ambao wana kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Simba katika uwanja wa Sokoine.

No comments