CHIRSTIAN BELLA AITOSA SHOW YA MOROGORO JUMAMOSI HII DAKIKA ZA MWISHO …kisa Fiesta


Unapoandaa onyesho katika msimu wa Fiesta linalohusu wasanii wanaotumika kwenye maonyesho hayo ya Fiesta, basi chukua tahadhari kubwa, yanaweza yakakusibu maumivu makubwa.

Mwimbaji supastaa wa muziki wa dansi Christian Bella, ameitosa show ya Morogoro iliyokuwa ifanyike Jumamosi hii ndani ya ukumbi wa Airport Pub.

Bella ameitosa show hiyo zikiwa zimesalia siku mbili tu kabla ya tukio hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Morogoro.

Mwandaaji wa onyesho hilo ameithibitishia Saluti5 kuwa onyesho hilo limeahirishwa dakika za mwisho kwa sababu zilizo nje ya uwezo wako.

Kisa cha Bella kuitosa show hiyo ni baada ya kujumuishwa kwenye onyesho kubwa la kuhitimisha maonyesho ya Fiesta ambalo litafanyika Leaders Club Jumamosi hii.

Tayari mji wa Morogoro ulishachafuka kwa matangazo ya kila namna kuanzia posters, vitambaa pamoja na yale ya radioni yaliyokuwa yananadi kwa nguvu onyesho hilo la Bella na bendi yake, lakini sasa mashabiki wa mji huo watalazimika kusubiri hadi wakati mwingine.

No comments