CHOCKY, ROGART, VICTOR NKAMBI WAIONGOZA TWANGA PEPETA KUITEKA KIGAMBONI IJUMAA USIKU


Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” jana usiku iliiteka Kigamboni baada ya kufanya onyesho la kutakata ndani ya ukumbi wa Savoy dot com ulioko eneo la Kibada.

Kwa vile Twanga pia ilikuwa na onyesho lingine kwenye ukumbi wa Bulyaga, Temeke, ilibidi iwatafute nyota wake wa zamani akiwemo Rogart Hegga, J Four Sukari, Hosea Bass, Adolph Mbinga na dansa Otilia kwaajili ya onyesho la Kigamboni.

Twanga hii iliyopiga Kigamboni chini ya unahodha wa Ally Chocky, pia ilipambwa na mpiga kinanda Victor Nkambi ambaye majuzi bosi wake Asha Baraka alitangaza kumsimamisha kazi kwa miezi miwili. Hii inaitwa ya Kaisari mwachie Kaisari.

Hili halikuwa onyesho la ‘ndondo’ bali lilikuwa onyesho rasmi ambapo mwenye ukumbi aliikodi Twanga Pepeta kwa taratibu zote za kiofisi.

Meneja wa Twanga Pepeta, Martin Sospeter alikuwepo ukumbini hapo kuhakikisha bendi yao inakidhi mahitaji ya mteja wao.

Nyimbo za Twanga Pepeta zikarindima mwanzo mwisho na kuwapagisha mashabiki waliofurika ndani ya ukumbi huo wa Savoy dot com. Ilikuwa show moja matata sana.

Kwenye drum alikuwepo  Emma Chocolate huku God Kanuti naye akiwa sehemu ya wacharaza magitaa.

Saluti5 ilishuhudia vyombo vya TOT vikitumika kwenye onyesho hilo na kutoa ‘sound’ iliyotulia sana.

No comments