CRISTIANO RONALDO ALIMPIGIA MESSI SIMU YA SIRI KUMFAHAMISHA KUWA ANASHINDA TUZO YA BALLON D'Or


Cristiano Ronaldo alimpigia simu Lionel Messi kumfahamisha kuwa atashinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon D'Or) mwaka huu, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.

Ukurusa wa mbele  wa kile kilichoonekana kama ni chapisho la jarida la France Football - ambalo ndilo linaloendesha tuzo hizo - uliwekwa kwenye mtandao wa Twitter, ukionekana kumbashiria Messi kama mshindi wa mwaka 2017.

Hata hivyo gazeti la Don Balon la Hispania linaripoti kuwa Ronaldo alimwambia Messi amefahamishwa ni yeye (Ronaldo) ndiye atakayekuwa mshindi.

Ronaldo atalingana na Messi kwa kutwaa mara tano tuzo hizo iwapo atakuwa mshindi wa mwaka huu. Mshindi wa 2017 atatangazwa rasmi Disemba 7.
No comments