DAMIAN MARLEY AKUMBUKA ALIVYOSISITIZWA ELIMU NA MAMA YAKE

STAA wa miondoko ya Reggae, Damian “Jr Gong” Marley amesema kwamba pamoja na kuzaliwa kwenye familia ya muziki lakini mama yake mzazi alimsisitiza sana juu ya umuhimu wa shule.

“Nimezaliwa kwenye familia ya muziki nikiwa na baba yangu, Bob Marley lakini mama yangu alikuwa muumini wa kupenda shule kuliko sanaa,” alisema rapa huyo.

“Katika mitaa ya mji wa Stone Hill tulipokulia kulikuwa na shule nyingi nzuri hivyo mama alinitaka nitumie muda mwingi kuzingatia masomo kuliko muziki,” aliongeza.

“Mama yangu pia alikuwa akitumbuiza miziki ya Jazz kwenye matukio mbalimbali, hiyo ikanifanya nijenge hamasa ya kupenda muziki zaidi.”


Damian ni mtoto wa nje ya ndoa wa hayati Bob Marley lakini hivi sasa amehamishia makazi yake nchini Marekani ambapo amekuwa akifanya vizuri kwenye muziki.

No comments