DANNY WELBECK AREJEA MAZOEZINI TAYARI KWA KUIVAA TOTTENHAM JUMAMOSI HII


Danny Welbeck amepigwa picha akiwa mazoezini akielekea kupona maumivu yake ya nyama za paja kuelekea mchezo wao wa watani wa jadi dhidi ya Tottenham Jumamosi hii.

Huku Olivier Giroud akiwa mashakani, Welbeck, 26 anaweza akawa miongoni mwa wa wachezaji wa Arsenal watakaoivaa Tottenham kwenye mchezo huo wa Ligi Kuu utakaopigwa dimba la Emirates.

Welbeck akiwa sehemu ya wachezaji wa Arsenal ambao hawakuwepo kwenye timu za taifa walioshiriki mazoezi Jumanne mchana kwenye ngome ya timu - London Colney.

Mshambuliaji huyo aliumia kwenye mchezo wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Watford Oktoba 14.
Arsenal star Danny Welbeck was pictured back in training after getting over a hamstring strain
 Danny Welbeck mazoezini siku ya Jumanne
With Olivier Giroud a doubt Welbeck could be in line for a return at the Emirates on Saturday
 Welbeck (kulia) akishiriki mazoezi ya Arsenal
First team stars Alexis Sanchez and Hector Bellerin were also involved in the session
Alexis Sanchez na Hector Bellerin na wakiwa mazoeziniNo comments