DAVID LUIZ KWISHA KAZI CHELSEA, CONTE ASEMA ANDREAS CHRISTENSEN NDIYO MPANGO MZIMA

Kocha wa Chelsea Antonio Conte ameweka wazi kuwa beki David Luiz anapaswa kuongeza bidii mazoezini vinginevyo atasugua benchi la wachezaji wa akiba au hata kuketi na mashabiki.
Mchezaji huyo wa miaka 30 hakujumuishwa kwenye kikosi cha Chelsea dhidi ya Manchester United Jumapili na hakuwepo hata kwenye orodha ya wachezaji wa akiba.
Kinda Andreas Christensen, rai wa Denmark mwenye umri wa miaka 21, ndiye aliyesimama kwenye ukuta wa Chelsea badala ya David Luiz.
Antonio Conte amesema hafahamu iwapo David Luiz atasalia Stamford Bridge msimu ujao.
"Lazima agangamale la sivyo atakuwa kwenye benchi au kwenye viti vya mashabiki,” alisema Conte pale alipoulizwa juu ya David Luiz
Kuhusu mustakabali wa Luiz, Conte akasema: "Sijui, ila Christensen ndiye tegemeo jipya la Chelsea kwa sasa na kwa siku za usoni”.


No comments