DAVID LUIZ MAMBO SI SHWARI KATI YAKE NA KOCHA ANTONIO CONTE ...huenda akasugua benchi dhidi ya Man United


Huenda beki David Luiz akaenguliwa kwenye mchezo muhimu wa Chelsea dhidi ya Manchester United kwa kile kinachoidaiwa kuwa ametibuana na kocha wake Antonio Conte.
Nyota huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 30, anaweza akageuzwa mbuzi wa kafara baada ya kipigo cha 3-0 kutoka kwa Roma ya Italia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumanne usiku.
Andreas Christensen huenda akasimama beki ya kati kuchukua nafasi ya David Luiz, mmoja wa wachezaji vipenzi wa mmiliki wa timu Roman Abramovich.
Chelsea na Manchester United zinakutana Jumapili hii katika mchezo muhimu wa Ligi Kuu ya England utakaochezwa kwenye dimba la Stamford Bridge. 


No comments