DAVIDO KUREJEA ZIMBABWE MWEZI DESEMBA KWA AJILI YA SHOO ILIYOVUNJIKA

STAA wa muziki nchini Nigeria Davido ambaye alilazimika kukatisha ziara yake ya muziki nchini Zimbabwe mwezi Oktoba baada ya kukamatwa akitakiwa kutoa maelezo polisi kufuatia kifo cha rafiki yake wa karibu, sasa atalazimika kurudi nchini Zimbabwe katika jiji la Harare mwezi Desemba mwaka huu.

Mastaa wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Jah Prayzah na Kutonga Kwaro ambao watakuwepo kwenye shooitakayofanyika katika ukumbi wa Harare International Comference Centre.


Kampuni ya "Concert Organisers" imethibitisha kufanyika kwa onyesho hilo baada ya kumalizana na Davido.

No comments