DEMU WA BECKHAM AKWEPA KUTUMIA “KILAJI”

MWANAMITINDO Victoria Beckham mwenye miaka 43, amekuwa akiagiza kahawa kwenye mitoko ya usiku ili kukwepa kupiga ulabu akihofia kuharibu maumbile yake.

Staa huyo ambaye mara kwa mara amekuwa akiongozana na mtoto wake wa kiume anayefuata nyayo zake, Brooklyn amesema kwamba anatumia kahawa yenye ladha ya ndizi ili kulinda afya yake.

Mwimbaji huyo wa zamani wa kundi la Spice Girls amesema kuwa angependa kuiambukiza tabia hiyo kwa watoto wake ili wasijitie kwenye matumizi mabaya ya pombe.


Victoria ni mke wa David Beckham ambaye amezaa nae watoto wanne ambao ni Brooklyn, Romeo, Cruz na binti yao Harper.

No comments