‘DOMO’ LA MOURINHO BADO LAMTESA KICHWANI BENZEMA TANGU 2011


JOSE Mourinho ndiye kocha anayeongoza kwa maneno na mara zote amekuwa akisemwa kuwa ni mropokaji, mwaka 2011 katika moja ya mikutano yake na wanahabari alitoa kauli ambayo haikumependeza moja ya mchezaji wake.

Alikuwa ni Karim Benzema na katika mkutano huo Mourinho alimfananisha Benzema na paka, kwani wakati  akifanyiwa mahojiano alisema kama nimekosa mbwa baasi nitakwenda kuwinda nikiwa na paka.

Kauli hiyo bado iko kichwani mwa Benzema na juzi wakati akiongea na jarida moja la michezo, alisisitiza kwamba tangu Mourinho atoe kauli hiyo, ndipo uhusiano wao ulianza kuvunjika.

Benzema anasema alikuwa akimuheshimu sana Mourinho lakini tangu amfananishe na paka heshima yake kwa kocha huyo ilianza kupungua na hakuwa anamuangalia vizuri toka kipindi hicho hadi sasa.

Karim Benzema amesema yeye ni kijana mpole sana lakini kama utamfanyia kitu hakipendi hawezi kuwa mpole tena ila kama utamuheshimu baasi heshima itakuwepo.


No comments