EVRA ATEMBEZA KUNG-FU KWA SHABIKI NA KULAMBWA KADI NYEKUNDU ...aweka rekodi mpya Europa Legaue


Beki wa Marseille ya Ufaransa, Patrice Evra alitolewa kwa kadi nyekundu hata kabla mchezo wa Europa Legaue dhidi ya Vitoria haujaanza.

Katika mchezo huyo uliochezwa nchini Ureno, shabiki mmoja wa Marseille aliyekuwa kwenye uzio wa uwanja wakati timu zikipasha moto na akamshambulia kwa maneno Evra akimshutumu juu ya kiwango chake kibovu msimu huu.

Beki huyo wa zamani wa Manchester United, hakuwa na hatua nyingine ya kufanya, zaidi ya kumpiga shabiki yule kwa staili ya Kung-Fu na kulambwa kadi nyekundu.

Bahati nzuri kwa Marseille ni kwamba Evra alikuwa mchezaji wa akiba katika mchezo huo na hivyo klabu yake ikaanza na wachezaji 11, lakini ikimwacha kocha Rudi García akiwa na upungufu wa wachezaji wa akiba.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Europa League tangu ilipoanza mwaka 2009 kwa mchezaji kutolewa kabla mchezo haujaanza.No comments