Habari

FABREGAS BADO ANAKOSA USINGIZI JUU YA NAMNA MOURINHO ALIVYOTIMULIWA CHELSEA

on

Ni miaka miwili imepita tangu kocha Jose Mourinho atimuliwe Chelsea, lakini bado hali hiyo inamtesa kiungo Cesc Fabregas.
Cesc Fabregas amefichua kuwa bado anakosa usingizi kwa namna kocha huyo alivyotimuliwa.
Mourinho alitimuliwa Chelsea takriban miaka miwili iliyopita ambapo Fabregas alikuwa mmoja wa wachezaji waliozomewa na mashabiki na kuitwa “panya” baada  Mourinho kutimuliwa kufuatia mwenendo mbovu wa kutetea taji lao la Premier League.
Kiungo huyo wa Chelsea amesema bado ana ukaribu na Mourinho licha ya kujiunga na Manchester United na bado anaendelea kuumizwa na msimu wa mwisho wa Mourinho ndani ya Chelsea.
“Wakati mwingine unakwenda kitandani lakini hupati usingizi kwa kufikiria mambo mengi, nashangaa peke yangu. Ilikuwa aibu kubwa,” anaeleza Fabregas katika mahojiano yake na BBC.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *