GUARDIOLA AMTAKA KIUNGO WA AJAX KIKOSINI MANCHESTER CITY

VINARA wa Ligi England, Manchester City wanahitaji saini ya kiungo wa kati wa timu ya Ajax, Frenkie de Jong mwenye miaka 20.

Man City wamepanga kukamilisha usajili huo katika dirisha dogo la mwezi Januari mwakani.


Kocha Pep Guardiola anataka kukitia makali kikosi chake akiwa anausaka ubingwa wa kwanza wa michuano ya Ligi ya England baada ya kutoka kappa msimu uliopita.

No comments