GUARDIOLA AMTOA MASHAKA ARSENE WENGER, AMWAMBIA REKODI HII NI YAKO HAKUNA WA KUIVUNJA


Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa timu yake haitoweza kuvunja rekodi ya mechi 49 bila kufungwa inayoshikiliwa na Arsenal na akamtaka meneja wa klabu hiyo kutokuwa na wasiwasi.

Arsenal ndiyo timu pekee iliyofanikiwa kumaliza msimu kwenye Premier League bila kufungwa hata mchezo mmoja, pale ilipotwaa ubingwa wa England mwaka 2003-04.

''Ningependa kumwambia Wenger kwamba rekodi hiyo ni yake hatutaweza kuivunja. Asiwe na wasiwasi'', alisema Guradiola.

Ikiwa ni mechi 10 zimechezwa na kila timu msimu huu, Wenger anasema ni mapema mno kudhani kuwa Manchester City itafikia mafanikio hayo.

No comments