HALI SI SHWARI CHELSEA, MKURUGENZI WA UFUNDI AACHIA NGAZI


Michael Emenalo amekatisha utumishi wake wa miaka 1o kama mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea, hatua inayozidi kutia mashaka hatma ya kocha Antonio Conte.

Habari za kung’atuka kwa Emenalo mwenye umri wa miaka 52 ambaye anatarajiwa kujiunga na Monaco, ni pigo kubwa kwa mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich.

“Huu umekuwa uamuzi mgumu kuuchukua, lakini ni uamuzi ambao naamini ni sahihi kwangu, kwa familia yangu na kwa timu,”
 Abramovich amekuwa akimwamini  Mnigeria huyo na alikuwa mmoja wa watu wacheche ambao ushauri wao ulikubalika kwa tajiri huyo wa Kirusi.

“Huu umekuwa uamuzi mgumu kuuchukua, lakini ni uamuzi ambao naamini ni sahihi kwangu, kwa familia yangu na kwa timu,” ilisema taarifa ya Emenalo iliyochapwa kwenye tovuti rasmi ya Chelsea.

Kuondoka kwa Emenalo pia kumegusa hisia za kocha Antonio Conte ambaye alisema: “Nasikitika Michael anaondoka Chelsea, napenda kumshukuru kwa kuniunga kwake mkono tangu nilipowasili kwenye klabu hii.

“Nilifurahia kufanya kazi na yeye, tulisherehekea pamoja ubingwa wa Ligi Kuu mwezi Mei. Namtakia kila la kheri.”

Chelsea imeshinda mataji matatu ya Ligi Kuu, taji la FA, League Cup, Europa League  na Champions League chini Emenalo.

Emenalo akiwa na Roman Abramovich
Emenalo aliyezungushiwa kiduara akiwa kwenye mchezo dhidi ya Manchester United Jumapili iliyopita

MAKOCHA WALIOPITA CHELSEA NDANI YA MIAKA 10  YA EMENALO 
Avram Grant (2007-08)
Luiz Felipe Scolari (2008-09)
Ray Wilkins (2009, kwa muda)
Guus Hiddink (2009, kwa muda)
Carlo Ancelotti (2009-11)
Andre Villas-Boas (2011-12)
Roberto Di Matteo (2012)
Rafael Benitez (2012-13)
Jose Mourinho (2013-15)
Steve Holland (2015, kwa muda)
Guus Hiddink (2015-16, kwa muda)
Antonio Conte (2016-)

WACHEZAJI WATANO WA BEI MBAYA WALIONUNULIWA CHELSEA CHINI YA  EMENALO
1. Alvaro Morata (Real Madrid, £70.6m)
2. Tiemoue Bakayoko (Monaco, £40m)
3. Michy Batshuayi (Marseille, £33m)
4. Diego Costa (Atletico Madrid, £32m)
5. Danny Drinkwater (Leicester, £30m)

No comments