HARRY KANE ASEMA: "NITAFIA HAPAHAPA TOTTENHAM"

MSHAMBULIAJI wa timu ya Tottenham, Harry Kane raia wa England amesema kuwa hana mpango wa kuondoka kwenye kikosi hicho cha jiji la London.

Kane mwenye miaka 24, amesema kuwa mpango wake ni kumalizia maisha yake ya soka kwenye kikosi hicho hivyo kufuta uvumi wa kuhamia Hispania kwenye timu ya Real Madrid.


Madrid wameweka wazi mpango wa kuwania saini ya Kane katika kipindi cha dirisha dogo la usajili lakini inaonekana kuna ugumu wa kumpata kwa sababu ya utata wa bei unaoweza kuibuka.

No comments