HASSAN MOSHI MTOTO WA TX MOSHI WILLIAM AMCHARUKIA DIAMOND NA MASHABIKI WAKE ...asema gari alilopewa Gurumo isiwe 'ishu'


MWIMBAJI wa  Msondo Ngoma Music Band, Hassan Moshi William, amefafanua kwamba kilichowakera zaidi kwa Diamond Platnumz na kundi lake la WCB ni dharau ya kuwaita “zilipendwa” huku wakitumia kionjo chao bila ridhaa.

Katika moja ya posti alizozitupia kwenye ukurasa wake wa Facebook, Hassan ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mwimbaji na mtunzi tegemeo ndani ya Msondo Ngoma, marehemu Tx Moshi William, amesema kuwa wao (Msondo) hawakuhitaji pesa kama wengine wengi wanavyodhani, bali walihitaji sheria za kunakili kazi zifuatwe kwa wahusika.

“Wabongo bhana dah wakati wimbo “Zilipendwa” unatoka nilipokea simu nyingi sana, oooh utakuwa ushachukua chako wewe hawawezi kufanya tu hivihivi now ndo haohao wanaichamba bendi, oooho mna njaa ninyi kwanza mmeshapotea msondo wenyewe wamekufa, kwasababu tu eti ni Diamond, dah jamani.”

“Waliopiga huo wimbo wote wapo na katika waimbaji aliyefariki ni mtunzi ambaye ni babaaangu Tx Moshi William,Maalim Gurumo na Joseph Maina tu,” ameandika Hassan.

“Kumbukeni hizo nyimbo zina hakimiliki, zinalipiwa kisheria na zimesajiliwa. Sasa mtu oooh alimpa gari Mzee Gurumo what's the f..k? Alimpa Gurumo kwa makubaliano yao binafsi na mapenzi yake hiyo haihusiani na kuchukua nyimbo ya bendi bila kuomba.”

 “Alichokosea Diamond ni kuiiita hii bendi “zilipendwa”, it means imepitwa na wakati wakati inaendelea kufanya kazi zake halafu unachukua vionjo vya hiyohiyo uliyosema zilipendwa unatumia kwenye nyimbo yako ya kisasa,” alifafanua Hassan kwenye posti hiyo.

Hivi karibuni Msondo Ngoma iliteka vichwa vya habari baada ya mwanasheria wao kuiandikia barua WCB kudai fidia ya shilingi milioni 300 kwa kutumia kionjo cha wimbo wao wa “Ajali” bila ridhaa yao.

Wimbo wa “Ajali” ulitungwa na TX Moshi William miaka 12 iliyopita, mwaka mmoja kabla hajafariki dunia.
Hiki ndicho alichoandika Hassan Moshi katika ukurasa wake wa facebook

No comments