HATIMAYE DAVID MOYES AUKWAA UKOCHA WA WEST HAM

David Moyes ameukwaa ukocha wa West Ham na ataanza majukumu yake ya kukinoa kikosi hicho Jumanne asubuhi.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United anartihi mikoba ya kocha aliyetimuliwa Slaven Bilic na  atakiongoza kikosi hicho hadi mwishoni mwa msimu huu.
Moyes aliyeishusha daraja Sunderland msimu uliopita, amepewa jukumu la kuhakikisha West Ham inabaki Premier League. Iwapo atafanikiwa hilo, atazawadiwa mkataba mpya wa miaka miwili.

No comments