HATIMAYE JAHAZI MODERN TAARAB YATANGAZA KUMREJESHA RAHMA MACHUPA


Jahazi Modern Taarab imetangaza kumrejesha kundini mwimbaji wake wa zamani Rahma Machupa akitokea kundi la Wakali Wao.

Hiyo ilitokea jana usiku ndani ya ukumbi wa Dar Live, Mbagala ambapo mashabiki wa Jahazi walilipuka kwa furaha pale Prince Amigo alipompandisha jukwaani  Rahma Machupa na kuweka wazi kuwa mwimbaji huyo amerejea nyumbani.

Rahma Machupa akaimba wimbo wake “Nipe Stara” ambao ulishangiliwa sana.

Akiongea na Saluti5, kiongozi wa Jahazi, Prince Amigo akakiri kuwa ni kweli Rahma Machupa amerejea kundini.

“Yeye mwenyewe ametuambia anataka kurudi nyumbani, hatukuwa na kizuizi tumempokea na sasa ni msanii wa Jahazi”, alisema Amigo.

Aidha, Amigo amesema milango bado iko wazi kwa mwimbaji yeyote wa Jahazi anayetaka kurejea kundini.
“Hatutamkataa yeyote anayetaka kurejea nyumbani, unaanzaje kumzuia mtu anayetaka kurejea nyumbani kwake?” alihoji Amigo.

Kwa upande mwingine mkurugenzi wa Wakali Wao, Thabit Abdul alipoulizwa na Saluti5 juu ya msanii wao kurejea Jahazi, alisema hana taarifa yoyote.

“Kwa kweli sijui chochote, wacha nifuatilie,” alisema Thabit Abdul.

No comments