HIVI NDIVYO MASHABIKI WA AL AHLY YA MISRI WALIVYOFURIKA MAZOEZINIKLABU ya Al Ahly ya Misri, imelazimika kukatisha mazoezi kuelekea mechi ya marudio ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca ya Morocco baada ya mashabiki kuvamia uwanja wakati walipojitokeza kusapoti mashujaa wao.

Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza nyumbani Alexandria, uongozi wa klabu uliamua kuwaalika mashabiki mazoezini ili kuwapa morali wachezaji, lakini mpango huo ukageuka kuwa balaa baada ya makumi ya maelfu kufurika ndani ya Uwanja wa Mokhtar El-Tesh jijini Cairo na kulazimika kusitisha mazoezi.

Inawezekana kuwa haukuwa mpango mzuri wa maandalizi, lakini bila shaka klabu imepata matumaini makubwa kuwa mashabiki wako nyuma yao na huenda wakawa msaada mkubwa wa kushinda mechi yao ya marudiano mjini Casablanca Jumamosi na kubeba ubingwa.

No comments