HIVI NDIVYO SANTI CAZORLA ALIVYONUSURIKA KUKATWA MGUU


Santi Cazorla anajiandaa kurejea uwanjani kuendelea kuitumikia Arsenal mapema mwaka ujao, hii ikiwa ni baada ya kuambiwa na madaktari kuwa huenda asiweze kutembea tena.

Kiungo huyo wa Kihispania  mwenye umri wa miaka 32, amekuwa akicheza na maumivu tangu alipoumia kifundo cha mguu mwaka 2013.

Akafanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu wake wa kushoto Disemba 2015, lakini akahitaji upasuaji mwingine mwaka mmoja baadae safari hii ikiwa ni mguu wake wa kulia.

Alicheza kwa mara ya mwisho Oktoba 2016 kabla ya kufanyiwa upasuaji mara nane, kidonda chake hakikupona na badala yake alianza kuugua.

Cazorla amesema madaktari walimwambia anafaa kushukuru sana iwapo ataweza kutembea tena baada ya kuambukizwa ugonjwa wa gangrini unaosababisha kuoza kwa sehemu ya mwili baada yake kufanyiwa upasuaji.

Cazorla ameambia gazeti la Marca kwamba ugonjwa huo ulikuwa "umekula" kano za kifundo cha mguu wake wa kulia.

"Sehemu ya ukubwa wa sentimita nane ilikuwa haipo," anasema.

Licha ya kutibiwa mara kadha kwa mafanikio, bado kulikuwa na wasiwasi kwamba mchezaji huyo wa zamani wa Villarreal na Malaga angepoteza mguu wake kutokana na maambukizi kwenye damu yake.

Mara ya mwisho kwake kufanyiwa upasuaji sehemu hiyo ilikuwa 29 Mei.

Wakati huo madaktari walipandikiza ngozi kutoka kwa mkono wake wa kushoto - ambayo ina tattoo - kwenye kifundo cha mguu wake wa kulia.

Tangu wakati huo, Cazorla amekuwa akishiriki mazoezi na amesema anatarajia kuwa sawa kwa kurejea dimbani mwakani.
The Arsenal midfielder has revealed what his achilles area looks like after eight surgeries
Kifundo cha mguu wa kulia kinavyoonekana baada ya kupona huku kikiwa na tatoo iliyotokana na kuhamishwa kwa nyama ya mkononi ili kutibu kidonda
A physio works on Cazorla's achilles as he bids to return to fitness before the end of the season
 Cazorla akifanyiwa mazoezi
Cazorla's tattoo has been party removed and can now be found covering his achilles area
Hii ndiyo sehemu ya tatoo ya Cazorla iliyohamishiwa mguuni

No comments