HIZI SI HABARI NJEMA KWA CHELSEA JUU YA KOCHA WAO ANTONIO CONTE


Italia inaangalia uwezekano wa kumrejesha tena kocha wa Chelsea Antonio  Conte ili akaifundishe  timu ya taifa ya nchi hiyo.

Timu ya taifa ya Italia inayojulikana kama "The Azzurri" haina kocha kwa sasa kufuatia kutimuliwa kwa Gian Piero Ventura mara tu baada ya kokosa tiketi ya kwenda Urusi kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018.

Shirikisho la soka la Italia limethibitisha kuwa Conte ni moja ya vipaumbele katika kuziba nafasi ya Ventura.

Rais wa FA ya Italia,  Carlo Tavecchio amesema kwa sasa makocha wanaowataka wako katika majukumu mengine lakini itakapofika mwezi Juni, watamchukua yule atakayekuwa huru.

Tavecchio akaviambia vyombo vya habari: "Tunaangalia kocha bora, mwezi Juni tunaweza kumpata mmoja wapo kati ya Ancelotti, Conte, Allegri, Ranieri na Mancini." 

Conte aliifundisha Italia mwaka 2014 hadu 2016 kabla ya kujiunga na Chelsea.


No comments