HOSEA BASS: TWANGA PEPETA NIACHENI KIDOGO NIBADILISHE UPEPO


Mmoja wa wacharazaji bora kabisa wa gitaa zito la bass, Hosea Mgohachi (Hosea Bass) ameamua kujiweka kando na bendi ya Twanga Pepeta.

Akiongea na Saluti5, Hosea akasema amejiengua kwenye kundi hilo takriban miezi miwili iliyopita, ili apate fursa ya kubadilisha upepo.

“Sijagombana na yeyote yule ndani ya Twanga Pepeta, ile ni bendi ninayoiheshimu sana, lakini kiroho safi niliwaomba waniache kidogo nibadilishe upepo,” alisema Hosea.

Hosea amasema kwa sasa yeye ni mwanamuziki wa kujitegemea anayefanya kazi na bendi yoyote ile kwa makubaliano ya kulipana kwa show.

“Nashukuru Mungu, rizki inapatikana, kazi zinamiminika vizuri”, aliongeza Hosea.

Kuondoka kwa Hosea kunamaanisha kuwa Twanga Pepeta imebakiwa na mpiga bass mmoja tu – Jojoo Jumanne.

No comments