HUSSEIN JUMBE ALIA NA AMRI YA MUZIKI MWISHO SAA SITA... asema "Makonda atatuua njaa mwaka huu"

KITENDO cha kutiwa matatani kwa mkongwe King Kikii kimeonekana kuchukua sura mpya baada ya wadau wengi kulalamikia kauli ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kuamuru muziki kuzimwa saa 6:00 usiku.

Mmoja wa wadau hao ni mwanamuziki wa siku nyingi wa miondoko ya dansi, Hussein Jumbe aliyesema kuwa anaamini kuwa agizo hilo la Makonda haliwezi kuwaacha salama wanamziki.


“Njaa ibishapo hodi mlangoni mapenzi huchomokea dirishani, kwa agizo hili la mkuu wa mkoa wa Dar Mh. Paul Makonda kuamuru muziki wa dansi upigwe mwisho saa 6 sisi wanamziki wa dansi tunatii amri hiyo lakini mmmh,” amesema Jumbe.

No comments