HUSSEIN JUMBE ASEMA SASA AMEAMINI UAMINIFU NI MTAJI... matapeli wakwamisha ujio wa studio yake

BOSI wa Talent Band, Hussein Jumbe amefichua kwamba mafundi ujenzi wamekwamisha mipango yake ya kufungua Studio kubwa ya muziki kwa mwaka huu, baada ya kukimbia na pesa za kumalizia jengo la studio hiyo.

Akiongea na Saluti5, Jumbe amesema jengo hilo (pichani juu), lilitarajiwa kukamilika na kuwa Studio ya kisasa zaidi ya kurekodia muziki tangu mwezi Juni, mwaka huu, lakini mafundi aliowaamini na kuwakabidhi pesa wamemuangusha.


“Mafundi niliowapa dhamana ya kunikamilishia jengo hilo la Studio wameingia mitini na mshiko, mimi nilipanga yangu kumbe Allah nae alishapanga yake, ama kweli uaminifu mtaji,” alisikitika Jumbe.

No comments