IBRAHIM AJIB ABWAGA MANYANGA KWA SHIZA KICHUYA

BAADA ya mfungaji wa Simba Shiza Kichuya kufikisha idadi ya mabao matano katika mechi za Ligi Kuu bara, staa wa Yanga Ibrahim Ajib amesema kwamba hana mpango wa kushindana na yeoyote na kwamba anachojali ni kuisaidia klabu yake kutetea taji la Vodacom.

Kichuya alifunga bao hilo lililozua utata kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City uliopigwa Jumapili iliyopita katika uwanja wa Sokoine.

Katika chati ya ufungaji hivi sasa, anaongoza Emmanuel Okwi mwenye mabao 8 kisha Mohamed Rashid 6 wakifuatiwa na Ibrahimu Ajibu na Shiza Kichuya wakiwa wamefungana kwa mabao 5 kila mmoja.

“Unajua mwisho mwa msimu kuna tuzo ya mfungaji bora lakini tangu mwishoni mwa Ligi nilistiza kuwa hayo sio malengo yangu, kipaumbele ni kuhakikisha nabeba taji nikiwa na Yanga,” alisema Ajibu.


Mabao matano ya Ajibu aliyafunga dhidi ya timu ya Njombe Mji, Ndanda, Kagera Sukari na Stand United huku Kichuya akizifunga timu za Ruvu Shooting, Mbao FC, Stand United, Yanga na Mbeya City.

No comments