IRINA SHAYK AKUMBUKA USALITI WA RONALDO

MREMBO Irina Shayk raia wa Urusi amesema kwamba hatasahau usaliti wa kimapenzi aliokuwa akifanyiwa na staa wa timu ya Real Madrid, Christian Ronaldo.

Penzi la wawili hao lilidumu kwa miaka mitano kabla ya wawili hao kutemana rasmi huku kila mmoja akishika njia yake.

“Nilimuamini sana mwanzoni lakini baadae nilianza kubaini usaliti baada ya kuona baadhi ya meseji za wanawake kwenye simu yake ya kiganjani” alisema mrembo huyo.

“Kulikuwa na mwanamke anayemtumia meseji za mara kwa mara kwenye simu yake hata nilipomuoji mwanzo hakuwa muwazi” aliongeza.

Staa huyo mwenye miaka 29 aliongeza kuwa kwa hivi sasa anahisi yupo kwenye penzi lililo salama zaidi tofauti na mwanzo.

No comments