J-LO, ALEX RODRIGUEZ MAPENZI HADI WIVU!

MAHUSIANO ya kimapenzi ya mastaa wawili Alex Rodriguez na Jeniffer Lopez yameanza kugeuka kituko baada ya kuonekana wakifatana kila eneo na wivu uliotawala kati yao.

Alex juzi uvumilivu ulimshinda ambapo alionekana kumfuata Jennifer Lopez kila eneo wakati mrembo huyo alipokuwa akirekodi matukio ya filamu ya Vanessa Hudgens katika jiji la New York.

Wawili hao baada ya tukio la kurekodi filamu walinaswa tena pamoja wakinywa wote mvinyo katika mgahawa wa Manhattan.

Jeniffer Lopez mwenye miaka 48 alishangazwa na ujio wa ghafla wa mpenzi wake, Alex Rodriguez mwenye miaka 42 katika eneo la kazi.


Mwimbaji huyo wa kibao cha "My Love Don’t Cost A Thing" alivaa koti lililoletwa na mpenzi wake kwenye eneo hilo walilokutana.

No comments