J4 SUKARI AFUNGUKA: "LUIZA MBUTU NDO KILA KITU KWANGU"

RAPA J4 Sukari amefunguka kuwa mkongwe wa kike wa muziki wa dansi, Luiza Mbutu amechangia kumfanya afike pale alipo kimuziki, hasa baada ya kutua ndani ya Twanga Pepeta, kwa kumpa ushauri na mbinu mbalimbali za mafanikio.

J4 aliyasema hayo jana mbele ya mashabiki waliokuwa wamefurika kuhudhuria shoo ya bendi hiyo iliyo chini ya Asha Baraka ndani ya Bulyaga Temeke wanakotumbuiza kila wiki katika siku za Ijumaa.
“Kiukweli kabisa, acha leo niweke wazi kuwa dada yangu Luiza Mbutu natakiwa nimpe heshima zote kwani amenisaidia kwa kiasi kikubwa hadi kufikia hapa kimuziki,” alisema J4.

"Yeye ndiye aliyenipa moyo sana nikiwa hapa. hata hili jina la J4 amenipa yeye na tangu kipindi hicho amekuwa msaada mkubwa kwangu katika kuhakikisha nafanya vizuri zaidi katika fani hii."


“Sina cha kukupa dada Luiza zaidi ya shukrani, lakini naamini Mungu anasikia namna ninavyokushukuru, natamani ubarikiwe zaidi na zaidi ili uweze pia kuwasaidia wengine wanaohitaji msaada kama ilivyokuwa kwangu,” aliongeza rapa huyo.

No comments