JAHAZI MODERN KUKINUKISHA KITUNDA, DAR LIVE WIKIENDI HII

JAHAZI Modern Taarab chini ya “Bosi Kichefuchefu” Prince Amigo Ijumaa hii wanatarajiwa kumwaga burudani pevu ndani ya Machimbo maeneo ya Kitundana Jumamosi dar Live, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam.

Prince Amigo aliyeongea na Saluti5 asubuhi hii amethibitisha kuwa kikosi chake kiko kamili kwa ajili ya kuhakikisha kinamwaga uhondo wa aina yake kwa wapenzi wao wa maeneo hayo.


“Tunawaomba mashabiki na wapenzi wetu wote wajitokeze kwa wingi katika kumbi zote tutakazotumbuiza wikiendi hii kwani tumewaandalia mambo matamu zaidi,” amesema Amigo.

No comments