JAHAZI MODERN TAARAB LEO HAKUNA KUREMBA DAR LIVE MBAGALA

ILE shoo maalum ya Jahazi Modern Taarab iliyovunjika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha Jumamosi iliyopita, inatazamiwa kudondoshwa usiku wa leo katika kiwanja kilekile cha Dar Live, Mbagala Zakheem, jijini Dar es Salaam.

Prince Amigo ambaye ndie bosi wa jahazi Modern, ameongea na Saluti5 muda mfupi uliopita na kuthibitisha kuwa kikosi chake kiko kamili kwa ajili ya kuhakikisha kinamwaga uhondo wa aina yake kwa wapenzi wao wa Mbagala na wilaya nzima ya Temeke leo.


“Tunawaomba mashabiki na wapenzi wetu wote wajitokeze kwa wingi ndani ya Dar Live leo ili kufaidi raha ambayo waliikosa wiki iliyopita, kwani tumewaandalia mambo matamu zaidi,” amesema Amigo.

No comments