JAMBO SQUAD, SAIDA KAROLI KUWASINDIKIZA MJENGONI CLASSIC


Joto la uzinduzi wa albamu ya ‘Afadhali’ linazidi kupanda ambapo wasanii Saida Karoli na kundi la Jambo Squad tayari wamethibitisha kushiriki.

Albamu ya ‘Afadhali’ ya bendi ya Mjengoni Classic itazinduliwa Jumamosi hii pale Olasity, Arusha.

Kiongozi wa bendi hiyo, Digitale Mukongya ameiambia Saluti5 kuwa katika orodha ya waalikwa amebaki msanii mmoja.

"Mama Saida Karoli atakuwa ndani ya nyumba, Jambo Squad wa hapa Arusha pia watakuwepo ...tunataka kuweka heshima na kufanya kitu tofauti," amesema.

Digitaly amesema video kwa ajili ya albamu hiyo imekamilika wiki iliyopita na itapatikana sambamba na CD ya nyimbo zao.

Mjengoni mbali na kuzindua albam hiyo itakuwa ikitimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

Bendi hiyo ina wakali kadhaa kama Sauti ya Radi, Donal Zinganguvu pamoja na Sele Mumba, Princess Jean ambao wamewahi kutamba na bendi mbalimbali hapa nchini.


Pichani juu ni mwimbaji wa Mjengoni Classic, Princess Jean

No comments