JAY Z, BEYONCE WAHAHA KUFUFUA PENZI LAO

BAADA ya kuwepo tetesi za kutopikikika chungu kimoja kwa muda mrefu, mastaa Jay Z na Beyonce wameripotiwa kuwa kwenye wakati mgumu wa kufufua penzi lao kama zamani.

Pamoja na ukweli kwamba walikuwa wakionekana mara kwa mara wapo pamoja nyakati za usiku, lakini ripoti zinadai kwamba ndani ya nyumba mambo yalikuwa tofauti kabisa.

Penzi la wawili hao limeanza kufuka tena ambapo sasa wamepania kuendelea kukusanya pesa kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko huko Mexico.


Beyonce na Jay Z uhusiano wao wa kimapenzi ulitajwa kuwa bora nchini Marekani kabla ya wawili hao kuanza kuzozana kufuatia tabia za mchepuko.

No comments