JIM IYKE AFUNGUKA KUHUSU TETESI ZA KUTOKA KIMAPENZI NA NADIA BUHARI

STAA wa Filamu za Nollywood, Jim Iyke amesema kuwa hakuwahi kutoka kimapenzi na mrembo wa Ghana, Nadia Buhari ambaye pia ni mcheza filamu.

Jim Iyke amesema kwamba alikuwa na ukaribu sana na Nadia lakini hawakuwahi kuwa wapenzi kama ambavyo uvumi umekuwa ukizagaa.
“Sisi ni watu wawili ambao tunafanya kazi pamoja kwa kiwanda cha burudani na mara nyingi tumekuwa tukishirikiana kizazi na sio mapenzi,” alisema staa huyo.


“Najua ukaribu wangu na Nadia ulisababisha watu watutafsiri vibaya lakini huo ndio ukweli hatukuwahi kuwa wapenzi kila mmoja anaheshimu mahusiano ya mwenzake,” aliongeza.

No comments