JOSE MOURINHO ASHANGAA POGBA KUMWACHIA ASHLEY YOUNG APIGE FREE-KICK


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amekiri kuduwazwa na kitendo cha kiungo Paul Pogba kumwachia Ashley Young apige mpira wa adhabu (free-kick) uliozaa bao la pili dhidi ya Watford.

Lakini Mourinho ameshangazwa zaidi na namna Ashley Young alivyouchonga kifundi mpira ule na kwenda moja kwa moja wavuni.

Pogba amekuwa akipiga mipira mingi ya adhabu, lakini akamruhusu Young akipige free kick dakika ya 29 na kutoa matokeo chanya.

“Katika umri alionao Ashley Young, anacheza soka la hali ya juu kuliko kipindi chochote kile, nina furaha nyingi juu yake,” alisema Mourinho baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu ya England uliosha kwa United kushinda 4-2.

No comments