JULIO AENDELEA KUUZA MANENO DODOMA FC

KOCHA mwenye maneno mengi wa timu ya Dodoma FC, Jamhuri Kihwelu “Julio” ametetea kiwango cha timu yake kwenye michuano ya Ligi daraja la Kwanza na kuwapinga wote wanaosema kikosi chake kinabebwa.

Julio amesema kuwa pamoja na uwepo wa lawama nyingi juu ya timu yake lakini ukweli ni kwamba wamejipanga vizuri ndio maana kinashinda mfululizo katika mechi zake.

“Sijui kwanini watu wanasema tunabebwa wakati ukiangalia mzunguuko wa kwanza tumeshinda mechi nyingi kwenye viwanja vya ugenini, hivyo sio kweli kuwa kikosi changu kinabebwa.”

Julio aliongeza kuwa anashukuru timu yake inaendelea kupambana na kukusanya matokeo mazuri kila kukicha na wakati huu hana muda wa kusikiliza lawama za watu wanaobeza timu yake.


Mara ya mwisho kikosi chake kilifanikiwa kuifunga Toto African mabao 2-1 na hapo ndipo lawama za kubebwa kwa timu hiyo zilianza kuchomoza.

No comments