JULIO ATETEA KIPICHO CHAO DHIDI YA PAMBA

KOCHA wa Dodoma FC ambao ni Kundi la vinara wa Kundi C katika michuano ya Ligi daraja la Kwanza nchini, Jamhuri Kihwelo "Julio" amesema kwamba hakuna timu inayoweza kushinda mechi mfululizo bila kupoteza na hii imekuja baada ya kushuhudia kikosi chake kikipoteza kwa bao 1-0 mbele ya Pamba.

Julio amesema kwamba imekuwa ni mazoea kwa klabu yake kuibuka na ushindi mfululizo lakini sasa ni zamu yao kusoma matokeo mabovu uwanjani.

“Ndiyo mambo ya mpira ukizoea kuzika ujue ipo siku na wewe utazikwa hili halikwepeki kwenye mambo ya soka kwasababu sisi sio wa kwanza kukumbwa na hali hii,”alisema Julio.

Kikoasi cha Pamba kilicheza soka safi mbele ya mashabiki wao kabla ya kupata bao katika kipindi cha pili baada ya kuwadhibiti wachezaji wa Dodoma FC katika idara zote.

Amos Mnyapi aliwainua mashabiki kipindi cha pili dakika ya nne kwa kufunga bao pekee lililodumu mpaka dakika ya mwisho.

Pamba waliingia katika mchezo huo wakiwa na alama 6 sasa wamefikisha alama 9 mara baada ya michezo 8 katika kundi lao C.

Makao hayo yanasababisha Kundi kuwa gumu ambapo Dodoma FC wana alama 18, Pamba alama 16 na Biashara wanasogea kwa karibu wakiwa na alama 14.


Katika michezo yote 14 ambayo kila timu itacheza katika makundi yote matatu zitatoka timu 6 ambazo zitapanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara msimu ujao.

No comments