KAGERA SUGAR YAJITOA MKIANI MWA LIGI KUU NA KUIACHIA ZAMU RUVU SHOOTING

SIKU chache zilizopita timu ya Kagera Sugar ilikuwa ikikamata nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu bara lakini sasa hivi mambo yamebadilika baada ya kuachia kijiti hicho kwa Ruvu Shooting.

Kagera juzi ilipata sre ya mabao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons hivyo kufikisha jumla ya alama 7 wakati Ruvu Shooting wataendelea kushika mkia wakiwa na alama 5 baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Azam FC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Mfungaji wa bao la Azam FC dakika ya 90 alikuwa kinda Yahya Zayed na sasa timu hiyo inafikisha alama 19 baada ya kucheza mechi tisa, ikiwazidi pointi mbili mabingwa watetezi Yanga.

Kipigo hicho pia kinaifanya Ruvu Shooting kuwa timu iliyo ruhusu idadi kubwa ya mabao ya kufungwa mpaka hivi sasa ikiwa imetikiswa wavu wake mara 14 huku yenyewe ikifunga mabao 3 tangu kuanza kwa Ligi.

Kikosi cha Azam FC kilikuwa na Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Aggrey Morris, Yakubu Mohammed, Idd kipagwile, Joseph Mahundi, Himid Mao, Salum Abubakar/Waziri Junior, Mbaraka Yusuph/ Peter Paul, Enock Atta Agyei na Yahya Zayd.


Ruvu Shooting kiliwasilishwa na Bidii Hussein, George Amani, Mau Bofu, Frank Msese, Shaibu Nayopa, Zuberi Dabi, Baraka Mtuwi, Shaaban Msala, Issa Kanduru/Said Dilunga, Ishala Juma/Jamal Soud na Abdulrahman Mussa.

No comments