KICHEKO MANCHESTER UNITED ...MARCOS ROJO AREJEA UWANJANI


Jumatano usiku, Marcos Rojo amerejea dimbani baada ya kuuguza maumivu kwa takriban miezi saba.

Sentahafu aliyeumia goti mwezi April, amecheza kwa dakika 45 kwenye mchezo wa wachezaji wa akiba dhidi ya Athletic Bilbao katika michuano ya International Cup.

Rojo hajakitumikia kikosi cha Jose Mourinho tangu mechi ya ushindi ya robo fainali ya Europa League dhidi ya  Anderlecht siku 209 zilizopita, usiku ambao mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic naye pia aliumia goti.

Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kurejea katika kikosi cha kwanza wiki tatu zijazo kwenye mchezo wa Champions League dhidi ya CSKA Moscow.

Marcos Rojo made his Manchester United return from injury on Wednesday night
Marcos Rojo ameitumikia Manchester United Jumatano usiku baada ya kupona goti
Rojo came through 45 minutes for the reserves against Athletic Bilbao in the International Cup
Rojo amecheza dakika 45 za kikosi cha wachezaji wa akiba dhidi ya Athletic Bilbao 
He played the entire first half as United reserves defeated their Spanish opponents 2-1
Rojo akishiriki mchezo dhidi ya Athletic Bilbao ambao kikosi cha akiba cha Manchester United kilishinda 2-1


No comments