KICHUYA ATETEA BAO LAKE LA "KUOTEA" DHIDI YA MBEYA CITY

WAKATI mchambuzi wa masuala ya soka kupitia kituo cha Azam TV, Ally Mayai akipinga bao la Shiza Kichuya lililoibeba timu yake ya Simba iliyokipiga dhidi ya Mbeya City jioni hii, mtazamo umekuwa ni tofauti kwa upande wa Kichuya mwenyewe.

Akiongea baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliokuwa umejaa msisimko wa aina yake, Kichuya amelilitetea bao hilo akisema kwamba lilikuwa ni halali.

“Lile bao ni halali na mambo mengine yote yanabaki kuwa ni ushabiki na mitazamo ya watu, naamini katika maamuzi ya refa na siwezi kuangalia wengine wanasema nini,” amesema Kichuya.

Kichuya ameibuka na kauli hiyo wakati tayari mchambuzi Ally Mayai ameshafafanua kwamba bao hilo lililowafanya Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilikuwa ni la kuotea.


Matokeo hayo ya leo yanaifanya Simba kuwa na pointi 19 na kuendelea kubaki Simba kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania bara ikifuatiwa na Azam FC ambayo nayo ina pointi 19 huku Yanga ikiwa katika nafasi ya tatu kwa pointi 17.

No comments