KIM KARDASHIAN, BEYONCE WAPOTEZEA BIFU LA MABWANA ZAO

WIKI iliyopita vimwana Kim Kardashian na Beyonce nao hawakubaki nyuma katika harusi ya mkali wa tenisi, Serena na walionekana wakizungumza pamoja kwa furaha, tofauti na baba za watoto wao ambao wana bifu.

Mtandao wa TMZ uliripoti kuwa Kim ambaye ni mke wa rapa Kanye West na Beyonce ambaye ni mama watoto wa Jay Z, walipokutana tu kwenye sherehe hiyo iliyofanyika New Orleans, walikumbatiana na kutafuta siti nzuri za kukaa VIP, wakaanza kupiga stori za hapa na pale.
Bifu la Jay-Z na Kanye West lilichangiwa na matukio mawili makubwa, Kanye kumshambulia Beyonce kwa maneno mwaka 2016 na mashtaka ya rapa huyo juu ya madai ya kutolipwa zaidi ya dola milioni tatu za huduma ya muziki wa mtandaoni ya Tidal (streaming).


Hata hivyo, urafiki huo wa ghafla wa Kim na Beyonce umetajwa kama njia ya kuwapoteza mapaparazi wanaoendelea kufuatilia kama bifu la Kanye na Jay Z limekita mizizi ama vipi.

No comments