KIWANGO CHA MESUT OZIL CHAWADUWAZA GARY NEVILLE NA THIERRY HENRYMesut Ozil alipewa heshima ya nyota wa mchezo katika mechi ya Ligi Kuu ya England dhidi ya Tottenham huku akiwaacha wachambuzi Gary Neville na Thierry Henry wakimimina sifa nyingi juu yake.

Kiungo huyo wa Kijerumani amekuwa akishutumiwa sana msimu huu kwa kiwango kisicho cha kuridhisha, lakini Jumamosi aliwafunga midomo waliokuwa wakimponda.

Akizungumza kupitia Sky Sports baada ya mchezo huo ulioshuhudia Arsenal ikishinda 2-0, Gary Neville, nyota wa zamani wa Manchester United, akasema: "Lazima kuna Mesut Ozil wawili maana huyu niliyemshuhudia leo sio yule niliyezoea kumuona katika siku za karibuni. Amekuwa bora sana leo."

Naye  Thierry Henry mshambuliaji wa zamani wa Arsenal aliyekuwa akichambua mchezo huo sambamba na Garry Nevile, akasema Ozil alitakata vilivyo.

"Namna alivyokuwa akisaidia safu ya ulinzi halafu baada ya muda mfupi unamkuta yuko mbele akikabiliana na kipa Hugo Lloris, ilikuwa ni jambo lililonivutia sana," alisema Henry.
No comments