KOCHA PSG ACHIMBA MKWARA KUWA NEYMAR HAYUKO SOKONI

Kocha wa Paris Saint-Germain, Unai Emery amesisitiza kuwa mchezaji wao Neymar aliyevunja rekodi ya usajili duniani, ataendelea kubakia na miamba hiyo ya Ufaransa.
Tetesi zilizo tawala duru za michezo katika mapumziko ya mechi za kimataifa, zimedai kuwa supastaa huyo wa Brazil hana furaha ndani ya timu hiyo aliyojiunga nayo mwezi August.
Gazeti moja la Hispania limeripoti kuwa Neymar aliwaambia wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona, Luis Suarez na Gerard Pique kwamba anajuta kuondoka Nou Camp.

Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos naye akakiambia kituo cha radio cha Cadena Ser kuwa Neymar anakaribishwa Bernabeu iwapo anataka kuondoka Paris.

Lakini kocha Emery amezitupilia mbali tetesi kutoka Real Madrid kwa kusema: "Wakati tulimpomchukua kutoka Barcelona, ilikuwa ni moja ya hatua sahihi, klabu na rais inamhitaji na ataendelea kubakia hapa."

No comments