KUMBE MWIGIZAJI OMOTOLA JALADE HAFAI KWA VIUNO... awaongoza wasanii wenzie kusakata muziki

WAKATI wa sherehe za utoaji wa tuzo za filamu nchini Nigeria katika ukumbi wa Eko jijini Lagos staa mwenye mvuto wa kimapenzi, Omotola Jalade aliongoza kundi la wasanii kucheza muziki.

Tuzo za mwaka 2017 za AFRIFF zimeshuhudia staa huyo pamoja na wengine wengi wenye majina makubwa wakitoka mikono mitupu na kuishia kucheza muziki ili kutumbuiza wageni.

Omotola alikuwa sambamba na Kate Henshaw, Ramsey Nouah, Kunle Afolayan, Chioma Chukwuka-Akpotha, Kunle Idowu, Olu Jacobs, Bolanle Austen-Peters, Ini Dima Okojie, Linda Ejiofor, Omoye Uzamere, Nonso Bassey na Fred Amata katika kutoa burudani ya muziki wakati wa zoezi la ugawaji wa tuzo.

Washindi wa tuzo hizo ni msanii Wulu kutoka Mali, Felicite wa Senegal na Hakkunde kutoka Nigeria ndio ambao walitawa tuzo hizo.

No comments