LADY GAGA AVISHWA PETE YA UCHUMBA NA MWANAUME WAKE MPYA

MWIMBAJI mtukutu wa kike, Lady Gaga inasadikika kuwa amevalishwa pete ya uchumba na jamaa yake mpya, Christian Carino mwenye miaka 48.

Gaga ambaye ametimiza miaka 31 alikubali ombi la kuvishwa pete tangu wakati wa majira ya kiangazi lakini hakutaka kuliweka jambo hilo wazi.

Jarida la “US Weekly” limeripoti kuwa wawili hao walishakubaliana kila kitu tangu mapema mwaka jana lakini walikuwa wakikwepa kupigwa picha na mwaandishi wa habari.


Pamoja na utukutu wa staa huyo lakini mwenendo wake umebadilika tangu aliponasa kwenye penzi la jamaa yake wa sasa.

No comments