LICHA YA KUITUNGUA MANCHESTER UNITED, KIBARUA CHA ANTONIO CONTE BADO HAKIKO SALAMA


MMILIKI wa klabu ya Chelsea, Roman Abramovich raia wa Urusi anahusishwa na mipango ya kuvunja mkataba wa kocha Antonio Conte ambaye aliwapa ubingwa wa England msimu uliopita.


Ndani ya timu hiyo kumetanda kiza kinene ambapo baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza hawako tayari kuona kocha wao anatupiwa virago.

Licha ya Chelsea kuitungua Manchester United 1-0 Jumapili jioni, inaaminika  Abramovich bado hakubaliani na falsafa za kocha huyo msimu huu.


No comments