LICHA YA KUKATAA KUSAINI MKATABA MPYA, MAN UNITED BADO HAIJAMKATIA TAMAA FELLAINIManchester United haitafanya hamaki ya kumuuza Marouane Fellaini mwezi Januari hata kama nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amekataa kusaini mkataba mpya Old Trafford.

Fellaini ambaye atafikisha umri wa miaka 30 wiki ijayo, amebakiza miezi saba na nusu kwenye mkataba wake wa sasa unaomwingizia pauni 120,000 kwa wiki.

Sheria zinamruhusu kuongea na vilabu vya nje ya England mwezi Januari kwaajili ya uhamisho uhuru wa dirisha la kiangazi.

Hata hivyo Manchester United bado haijakata tamaa na inaaminika inaendeleza juhudi za kumshawishi badala ya kufikiria kumpiga bei mwezi Januari.
No comments