Habari

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA (VPL), HII HAPA TENA WIKIENDI HII

on

Mechi moja inachezwa
kesho Ijumaa Novemba 3, 2017 kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ambako
mwenyeji Majimaji FC itacheza na Stand United ya Shinyanga.
Mchezo huo wa Songea
utaanza saa 10.00 jioni (1600h).
Jumamosi kutakuwa na
michezo mitano ambako minne itaanza saa 10.00 jioni (1600h) wakati mwingine utakuwa
saa 1.00 usiku (1900h).
Michezo hiyo ya
Jumamosi itakuwa ni kati ya Singida United itakayocheza na Young Africans
kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida wakati Tanzania Prisons itakuwa wageni
wa Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba 
mjini Bukoba, Kagera.
Njombe Mji kwa upande
wake watakuwa wenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani
Njombe huku Mtibwa Sugar ikisafiri kutoka Morogoro kwenda Mtwara kucheza na
Ndanda FC kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona. Hizo ni mechi zitakazochezwa saa
10.00 jioni.
Mchezo pekee
utakaofanyika saa 1.00 usiku utakuwa ni kati ya Azam FC na Ruvu Shooting kwenye
Uwanja wa Azam.
Jumapili kutakuwa na
michezo miwili ya Ligi Kuu ambako Lipuli ya Iringa itakuwa mwenyeji wa Mwadui
FC ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Samora wakati Simba itakuwa mgeni wa Mbeya
City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mechi hizo zitaanza saa 10.00
jioni.

CHANZO: TFF

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *